Njoni Tumwimbie
- Anonymous
- Nov 17, 2023
- 1 min read
Njoni, tumwimbie na kumshangilia, njoni,
tumwabudu Bwana.x2
1. Njoni tumjongee njoni kwa masifu -Njoni, tumwabudu Bwana
2. Tumfanyie shangwe mwamba wa wokovu- Njoni, tumwabudu Bwana
3. Yeye ndiye Bwana yeye Mungu mkuu- Njoni, tumwabudu Bwana
4. Yeye ndiye mfalme wa wafalme wote- Njoni, tumwabudu Bwana
5. Milima ni yake pia makorongo- Njoni, tumwabudu Bwana
6. Bahari ni yake pia nchi kavu- Njoni, tumwabudu Bwana
7. Yeye Mungu wetu aliyetuumba- Njoni, tumwabudu Bwana
8. Sisi ndiyo watu wa malisho yake- Njoni, tumwabudu Bwana

Comments