Njooni Tumfanyie Shangwe
- Benard Mukasa
- Oct 19, 2023
- 1 min read
Updated: Dec 23, 2023
Njooni tumfanyie shangwe Mungu wetu- Njooni tumfanyie shangwe Mungu wetu, Jiungeni wote tuimbe pamoja- Njooni tumfanyie shangwe Mungu wetu Kwa miondoko ya raha na kucheza - Njooni tumfanyie shangwe Mungu wetu, Kwa ngoma safi tamu na za midundiko - Njooni tumfanyie shangwe Mungu wetu
Bwana ametenda wema wa ajabu - Njooni tumfanyie shangwe Mungu wetu Machozi ameyageuza vicheko - Njooni tumfanyie shangwe Mungu wetuTumwimbie leo tumsifu yeye - Njooni tumfanyie shangwe Mungu wetu Tukipigapiga vifua kwa maringo - Njooni tumfanyie shangwe Mungu wetu
Tumpungieni mikono kwa madaha - Njooni tumfanyie shangwe Mungu wetu Ajue kwamba leo tumefurahi - Njooni tumfanyie shangwe Mungu wetu Na shingo zinesenese kwa midundo - Njooni tumfanyie shangwe Mungu wetu mwili uyumbeyumbe kushoto kulia - Njooni tumfanyie shangwe Mungu wetu
Watoto nao wabebwe juu juu - Njooni tumfanyie shangwe Mungu wetu Wajue kwamba Mungu anawapenda - Njooni tumfanyie shangwe Mungu wetu Umati wote urukeruke juu - Njooni tumfanyie shangwe Mungu wetu Tusisite Mungu yu katikati yetu - Njooni tumfanyie shangwe Mungu wetu

Comments