top of page

Nota Mpaka Mbinguni

Updated: Dec 21, 2023



Tutamsifu Mungu, tutamwimbia Watunzi tutampangia nota mpaka mbinguni

Usiku na mchana, jioni na asubuhi Kiangazi masika mpaka Mbinguni


  1. Tumetafiti tukauliza, maandiko tukafunua Kutambua watakatifu, wanafanya kazi gani Mbinguni

  2. Enyi wasomi tuambieni, wanasayansi tujibuni Katika mambo ya mbinguni, nini kinafanyika duniani

  3. Tumetambua kule mbinguni, hakuna kwenda ofisini Wala kumbi za burudani, hata kilimo hakuna lakini

  4. Kumbe furaha za dunia hii, ni upumbafu ni wazimu Na anasa za maadili, sisi waimbaji tumeamua

  5. Waamini wote furahini, makasisi shangilieni Nanyi watawa jiungeni, kwa waimbaji hakuna matata

  6. Upendo wake ni wa ajabu, fadhili zake za milele Huruma yake ni amini, msamaha wake unashangaza

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating

Recent Posts

bottom of page