Nyota ya Bahari
- Alfred Osonga
- Oct 13, 2023
- 1 min read
Updated: Dec 23, 2023
Bara na bahari furahini sana Tumemulikwa na nuru ya Mbinguni Bara na bahari furahini sana Tumemulikwa na nuru ya Mbinguni
Pendo lako mama, limetuvutia, Tunatangaza sifa zako kwa nyimbo Bara shangilia, bahari ivume, Tumsifu mama, mama wa Maulana
Piga tarumbeta, pigeni mluzi, Imbeni wimbo wa mama wa Mulungu chezeni pamoja, ruka juu juu, Mama wa Yesu afurahi Mbinguni
Mama wa Mwokozi, Malkia wa Mbingu Mwanga anamu somo wa kwaya yetu uliyekingiwa dhambi ya asili, Daraja letu tuendao Mbinguni
Nyota za angani zamulika nchi, Mama Maria anamulika nyoyo usiku mchana anatuangaza, Tunatembea na nuru siku zote

Comments