Nyota ya Bahari
- Alfred Osonga
- Oct 21, 2023
- 1 min read
Updated: Dec 23, 2023
Bara na bahari furahini sana- Tumemulikwa na nuru ya Mbinguni, bara na bahari furahini sana- Tumemulikwa na nuru ya Mbinguni
Pendo lako mama, limetuvutia- Tunatangaza sifa zako kwa nyimbo bara shangilia, bahari ivume -Tumsifu mama, mama wa Maulana
Piga tarumbeta, pigeni mluzi- Imbeni wimbo wa mama wa Mulungu chezeni pamoja, ruka juu juu- Mama wa Yesu afurahi Mbinguni
Mama wa Mwokozi, Malkia wa Mbingu- Mwanga anamu somo wa kwaya yetu, uliyekingiwa dhambi ya asili- Daraja letu tuendao Mbinguni
Nyota za angani zamulika nch- Mama Maria anamulika nyoyo, usiku mchana anatuangaza- Tunatembea na nuru siku zote

Comments