Nyota ya Mashariki
- Benard Mukasa
- Oct 19, 2023
- 1 min read
Updated: Dec 23, 2023
Kakukirimia, uwe ulivyo, Atakutumia impendezavyo Akikuinua, inuka, hivyo, Ninakuombea heri vilivyo; Hakunipa hayo, nikuhitaji, Kwa niliyo nayo, upate maji, Na mwisho wa hayo, tuvikwe taji, Tuingie nayo, wa mbingu mji.
Sirudi kwa njia, yake herode, Anakuvizia, kila upande, Wivu unamjia, kakunja, konde, la kukuzuia juu usipande; Ni kama Kaini, mwua Abeli, au Raubeni, wa Israeli, Waliotamani, kuzika, hali, Ya wadogo duni, wake Jalali!
Ninakuombea, usife moyo, Maana dunia, si rafikiyo, Wewe fuatia, za Kristu, nyayo, Aliyekufia, kwa mizigoyo; Wa ulimwenguni, watakufumba,Wazuri machoni, moyo mwembamba, Hawatatamani, uitwe, mwamba,Ni wivu moyoni, unawasomba!

Comments