Nyota ya Matumaini
- Pascholas Nestory
- Nov 1, 2023
- 1 min read
Updated: Jan 14, 2024
Mama yetu maria, ni mama wa neema, tena ni kimbilio la watu wote wakosefu, ni msaada wa kweli mama tuombee.
Ni nyota, ni nyota, mama yetu maria ni nyota ya matumaini x2
Mlango wa mbingu, sanduku la agano, malkia wa amani, malkia mwenye huruma, mama mpendelevu mama tuombee
Nyota ya asubuhi, ni mnara wa pembe, kimbilio la wakosefu mama tuombee, mama yetu maria kiongozi wetu.
Twakushukuru mama, kwa maombezi yako, na kwa neema zote unazo tuombea mama, malkia wa amani mama tuombee.

Comments