top of page

Nyumbani Mwake Bwana

Njoni tumsujudu yeye aliyetuumba Yeye anatawala kwa haki na uamini x2


Yeye ni Mungu mwenye utukufu wa ajabu Yeye ni Mungu mwenye radhi nyingi na rehema.


Bwana ni mtawala amejaa utukufu na mashuhuda yake yastahili imani.


Yeye ni Mungu wetu wa amani na mapendo Yeye ni Mungu mwenye utukufu wa ajabu.


Tumpigie shangwe mwamba wa wokovu wetu Ni Mungu wa ujuzi na ni Mungu wa fahamu.


Na kwa nyimbo za sifa tujongee uso wake Vifijo na nderemo tumsifu Mungu wetu


Na enyi waadili tukuzeni jina lake Mfanyieni shangwe yeye aliyetuumba.

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating

Recent Posts

bottom of page