top of page

Ona Mnavyopendeza

Ona mnavyopendeza,

ona mnavyometameta x2

Wapenzi wana harusi

mwende mkaishi salama x 2


Kwenye maisha ya ndoa,

kuna raha pia tabu,

mkiishi kwa upendo tabu na raha ni sawa.


Mpendane siku zote,

katika maisha yenu,

msiruhusu shetani kuvuruga ndoa yenu.


Watoto mtakaopewa,

muwatunze hao vyema,

kwani kufanya hivyo Mungu mtampendeza.


Mjenge familia bora,

yenye kuheshimu sala,

kwani kwa njia ya sala tunaongea na Mungu.

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating

Recent Posts

bottom of page