top of page

Pendo La Ajabu

Updated: Dec 25, 2023


Bwana pendo gani wewe (ukanipa) kwa kunifilia mimi (msalabani) hilo pendo lako Bwana (la ajabu) nami ninasema asante, (kwani pendo lako Ewe Yesu) halihesabu mabaya, (siku zote linavumilia) tena halinung'uniki, (hata siwezi kulieleza) pendo lako la ajabu {(kwa) maneno yangu (mimi) siwezi kabisa (ku) eleza jinsi unavyonipenda x2} Basi ninaahidi Yesu (kukutumikia) mimi na familia yangu (sote kwa pamoja) Tutatangaza jina lako (ili watu wote) wakujue wewe mfalme

  1. Ulinikomboa kwa njia ya kifo pale msalabani, kwa uchungu mwingi, aibu aibu Bwana ulipata kwa sababu ya kunipenda mimi.

  2. Maadui zangu wanashangaa sana kwa jinsi gani unavyonipenda, hakika we Bwana ni rafiki mwema wanipenda sana

  3. Ulipofufuka ulikamilisha uokovu wangu hapa duniani na pia mbinguni

  4. Yesu nakupenda we mpenzi wangu, umevumilia uovu wangu, Bwana penzi lako ni la ajabu mno halijui mabaya ladumu siku zote Bwana.

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating

Recent Posts

bottom of page