top of page

Pokea Zawadi Zetu

Pokea zawadi zetu Baba x2


Mkate na divai pokea Baba

Mazao ya mashamba upokee


Na kiini cha ngano pokea Baba

Na tunda la mzabibu upokee


Pokea mali yetu pokea Baba

Na pia nafsi zetu upokee


Furaha na uchungu pokea Baba

Fanaka na udhiki upokee


pokea fedha zetu pokea Baba

Ingawa ni kidogo upokee


Tazama nia zetu pokea Baba

Kwa radhi zako upokee


Kwa moyo mkunjufu pokea Baba

Twatoa vyote kwako upokee


Vipate kuugezwa pokea Baba

Viweze kutufaa upokee.

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating

Recent Posts

bottom of page