top of page

Rarueni Mioyo Yenu

Updated: Dec 23, 2023

Rarueni mioyo yenu, wala (wala) si mavazi yenu x2

  1. Mrudieni Mungu, Mungu mwenyezi, amejaa huruma, huruma na neema rarueni mioyo yenu.

  2. Mwenyezi Mungu, hachukii upesi, mwingi wa fadhili, tayari kusamehe rarueni mioyo yenu.

  3. Huko sayuni, pigeni tarumbeta, waamuru watu wote wafunge, rarueni mioyo yenu.

  4. Wakusanye watoto, hata na wanao nyonya, na maharusi, toka nyumbani mwao, rarueni mioyo yenu.

  5. Mlango wa hekalu, mpaka, madhabahuni, makuhani, walie na kuomba, rarueni mioyo yenu.

  6. Ndipo mwenyezi ataipenda nchi, atawahurumia, hawa watu wake, rarueni mioyo yenu.

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating

Recent Posts

bottom of page