top of page

Sasa ni Wakati Mzuri

Updated: Dec 25, 2023


Sasa ni wakati mzuri twendeni madhabahuni, Tukatoe sadaka zetu, tulijenge kanisa la Mungu, (Ewe ndugu yangu mkristu, Changamka, changamka, peleka sadaka kwa Bwana Nenda katoe kwa moyo mweupe uzipate baraka za Mungu) x2

  1. Mkristu kutoa sadaka, Ndio wajibu wa kila mmoja, Hivyo mkristu kumbuka wajibu, Nenda katoe sadaka kwa Bwana.

  2. Mwambie Bwana Mungu wako, Baba pokea nilichokileta, Hiki ndicho ulichonijalia, Nakutolea kama shukrani.

  3. Zamani za mababu zetu, Walipeleka sadaka za nyama, Nasi wakristu wa leo twendeni, Tupeleke fedha za mifukoni.


Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating

Recent Posts

bottom of page