top of page

Sikiliza ni Mpendwa Wangu

Updated: Dec 19, 2023

Sikiliza ni mpendwa wangu, ni mpendwa wangu tazama anakuja. x2

Akirukaruka milimani, akichacharika vilimani, mpendwa wangu ni kama paa, ni kama ayala tazama anakuja x2

  1. Tazama tazama asimama, asimama nyuma ya ukuta wetu, anachungulia dirishani, atazama kimiani anakuja.

  2. Mpendwa wangu alinena, yeye alinena akaniambia, ondoka ewe mpenzi wangu, ewe mzuri wangu ili uje zako.

  3. Nitazame nitazame uso wako, niisikie sauti yako, maana sauti yako tamu, ni tamu na uso wako ni mzuri.

  4. Mpendwa wangu kweli ni wangu, hakika ni wangu na mimi ni wake, mpendwa wangu ulisha kundi,kulisha kundi lake kwenye nyinyolo.

  5. Hata jua lipungue kweli, na vivuli vyote pia vikimbie, unigeukie mpendwa wangu, unigeukie ewe mpendwa wangu.

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating

Recent Posts

bottom of page