Simameni Watu Wote
- Alfred Osonga
- Nov 17, 2023
- 1 min read
Updated: Dec 23, 2023
Simameni watu wote leo katika nyumba ya Bwana (wote) furahini mbele zake Bwana imbeni nyimbo za shangwe
(shangilieni) vigelegele pigeni makofi hekaluni mwake mwimbieni Bwana wimbo mpya (watu wote). x2
Akina mama wote (hoye) akina Baba wote (hoye) njooni wote mbele za Bwana, mkiimba nyimbo za shangwe, njooni wote, mbele za Bwana njooni leo mbarikiwe. x2
Enyi vijana wote (hoye) enyi wazee wote (hoye) njooni wote mbele za Bwana mkiimba nyimbo za shangwe, njooni wote mbele za Bwana njooni leo mbarikiwe. x2
Ni siku ya furaha (leo) ni siku yenye heri (leo) tumshukuru muumba wetu Mungu, tumsifu Mwenyezi Mungu.x2

Comments