top of page

Usia wa Maria

Updated: Dec 2, 2023



Sisi wana dunia tukumbuke maneno, aliyosema Bikira Maria, Alipowatokea watoto wa Fatima, Lucia Francis na Jacinta, Alisema tusali, tusali rosari, tupate amani, Na tuwaombee wale wakosefu wasio na mwombezi, Na wasiomwamini Yesu Mwokozi wamuamini ili waokoke


Mama yetu anahuzunishwa sana, na matendo yetu maovu,

Anajua adhabu yetu ijayo, hivyo anaona huruma sana


Atusihi tuache dhambi kwa dhati, tuache kumkosea Yesu,

Tuyatubu makosa yetu yote, ili Bwana atupatie amani


Tusitende maovu na dhambi, atusihi mama wa Yesu, Tusimkasirishe tena Mungu, asije tutupa motoni milele


Ibada ya moyo safi wa Maria, tuizingatie daima, Tupokee komunio takatifu, kila Jumamosi ya kwanza ya mwezi

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating

Recent Posts

bottom of page