top of page

Sote Tufurahi

Sasa yametimia yaliyotabiriwa, Mwokozi kazaliwa.

Sote tufurahi Habari ni njema

Njoni, nyote, wahi Tupate uzima


Kule Bethlehemu Ni Yesu kazawa

Mama Mariamu Alivyoambiwa


Kumbe, huyo Mwana Kalazwa horini

Huyo, Yesu Mwana Akawa shidani


Mwana atiiye Ni Bwana shujaa

Kwake tuwe wana Ni mponya dunia


Jeshi la mbinguni Katoa injili

Watu malishoni Kaona ni kweli


Mungu yuko nasi Katika dunia

Pendo kwa waasi Katoa kwa nia


Raha na tushike Tunaye Masihi

Haya twende kwake Sauti zasihi

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating

Recent Posts

bottom of page