top of page

Taji Mvikeni

  • Hymns
  • Nov 6, 2023
  • 1 min read

Taji mvikeni Taji nyingisana, kondoo mwake Kitini,

Bwana wa mabwana; Nami tamsifu Alikufa kwangu,

Ni mfalme mtukufu, Seyidi wa mbingu.


Taji mvikeni Mwanawa bikira; Anazovaa kicwani

Aliteka nyara; Shilo wa manabii Mchunga wa watu

Shina na tanzu vya Yese Wa Bethilehemu.


Taji mvikeni Bwana wa mapenzi; Jeraha zake nishani

Ni vito vya enzi, Mbingu haina Hta malaika

Awezaye kuziona pasipo kushangaa!


Taji mvikeni Bwana wa Salama; Kote-kote duniani

Vita vitakoma; Nayo enzi yake Itaendelea,

Chini ya miguu yake, Maua humea.

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating

Recent Posts

bottom of page