Tazama
- Deo Kalolela
- Oct 12, 2023
- 1 min read
Updated: Dec 25, 2023
Tazama Bwana tunakuja kwako (leo) twaleta sadaka zetu mbele yako, tunakuombaMungu Baba pokea x2
Kwa nguvu zako uliweza kustawisha mazao bora na sasa twakutolea, Mashamba uliyarutubisha kwa mvua nzuri mazao kwa wingi yakasitawi
Bahari mito na maziwa Bwana ukajaza samaki wengi wa kupendeza, Angani ndege wengi wanarukaruka kushangilia neema yako Ee Bwana.
Wanyama maporini wakarukaruka kushangilia neema yako Ee Bwana, Wadudu nao wakachezacheza kuonyesha furaha kubwa waliyo nayo

Comments