top of page

Tazameni Karamu ya Bwana

Updated: Dec 25, 2023


Tazameni karamu ya Bwana iko mezani [mbele], ni karamu ya upatanisho na amani [kwetu] (Haya ndugu simama [ndugu] ewe mkristu jongea [mbele] x2Yesu Kristu anatualika kwa chakula bora cha uzima x2)

  1. Ndugu tazama Yesu anatualika, na wewe kwanini moyo wako unasita Vikwazo gani vinavyokusonga moyo,hata ukatae mwaliko wa Bwana Yesu

  2. Hebu tazama wenzako wanavyokwenda,kwa heshima kwa upole na unyenyekevu, Nyoyo zao ni safi nyuso za furaha,wanaishiriki vema karamu ya Bwana.

  3. Ewe mkristu utafiti moyo wako,kama una dhambi nenda Ukaziungame,Kwa nini unakuwa mtumwa wa dhambi,acha dhambi tenda mema ili uokoke.

  4. Haya shime twendeni Bwana atuita,tukashiriki pamoja karamu ya Bwana. Waumini wote wenye mioyo safi,ni wapenzi wake Yesu Kristu Mkombozi

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating

Recent Posts

bottom of page