Tu Wafalme
- Hymns
- Nov 1, 2023
- 1 min read
Updated: Dec 27, 2023
Tu Wafalme, tumeleta toka mbali tunu zetu, milimani mabondeni nyota twafuata
Nyota hio ya ajabu nyota hio yenye nuru- Itulete Bethlehem kwenye nuru kamilifu
Hii dhahabu nimeleta yuko Mfalme Bethelehemu itafaa kwa taji lake Mfalme wa milele,
Huu uvumba nimeleta, kuonyesha ndiye Mungu-msifuni na kumwomba enyi wanadamu
Manemane nimeleta, ni dalili ya mateso kwa mauti ni tayari, kwa kaburi lake
Mtukufu amekuja,Mfalme Mungu na dhabihu, Aleluya, aleluya wote humwimbia.

Comments