Tumeingia Kwako Bwana
- Alfred Osonga
- Oct 28, 2023
- 1 min read
Updated: Dec 23, 2023
Unison)Tumeingia kwako Bwana, tunaimba kwa furaha nyumbani mwako. x2 Tuko mbele zako asubuhi tumekuja
Nyumbani mwako Mungu Baba utupokee utubariki x2
Kwa shangwe kubwa vigelegele na nyimbo Baba tumekuja-hekaluni mwako. kwa vinanda kwa vinubi kwa machezo Baba tumekuja –hekaluni mwako.
Bwana ututakase sisi wanao leo asubuhi-Altareni mwako, Bwana utujalie baraka zako leo asubuhi- Altareni mwako.
Nyumba yako ni nyumba ya sala tumekuja tupokee-utusikilize. Dua zetu maombi yetu na sala zetu zipokee-utusikilize.
Nyua zake Bwana kweli zapendeza macho njooni nyote-njooni tumwabudu, ingieni malangoni mwake kwa furaha tumwabudu- leo na milele.

Comments