Tunakuomba
- Anonymous
- Nov 18, 2023
- 1 min read
Tunakuomba, upokee Baba Zawadi zetu leo hii
Sisi wanao tunaleta kwako Zawadi zetu leo hii
Mkate na divai, mavuno ya shamba Tunaomba upokee, hata nafsi zetu Tunakutolea tunaomba upokee
Vipaji vyetu twavileta
Uvibariki uvitakase
Vipaji vyetu vigeuze
Vifanye viwe mwili na damu
Utujalie afya nzuri
Tuendelee kufanya kazi
Msaada wako twauomba
Kwenye maisha ya kila siku
Uibariki misa yetu
Na sala zetu, na nyimbo zetu
Nasi wenyewe tubariki
Utufikishe huko mbinguni

Comments