top of page

Tutangaze Neno

Karibuni wakristu, sote tujiandae, wakati umefika sasa wakutangaza neno

Ni neno la uzima, neno toka kwa Bwana, hakika, ni chakula kweli kinashibisha roho.


1. Ni neno toka kwa Bwana, Ni neno lenye uzima

Ni neno lenye wokovu, karibu tushiriki.


2. Atakayo nena nawe, atakayokuamuru,

Yashike kwa moyo wako, na uwe mtiifu.


3. Kwa kuwa ni Mungu kweli, ndiye kimbilio letu,

Mwamba wa maisha yetu, aliye mwaminifu.

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating

Recent Posts

bottom of page