top of page

Twakukimbilia Maria

Twakukimbilia Maria, Mama Bikira mwenye huruma

tutie nguvu ya safari tufike Kwa mwanao Yesu Kristu

Angaza njia mama Maria Tufike makao ya uzima

Giza limeyafunika macho mama Maria Mama Maria twapotea

Tunahitaji msaada wako mama Maria Mama Maria tuone njia


Safari ni ngumu Maria Shetani mwovu atusumbua

Hatua ni nzito Maria Miguu yetu imelegea


Utupe nguvu Maria Ili tusije vunjika moyo

Tuwe shupavu na imara Katika safari hii ya roho


Utuombee kwa mwanao Tupate nguvu kumshinda shetani

Tujikane tujute dhambi Tuweze kufika kwake mbinguni

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating

Recent Posts

bottom of page