top of page

Twende Wote Aste Aste

Updated: Dec 21, 2023



Twende wote aste aste na sadaka mikononi vipaji mbalimbali twende wote kwa furaha, Mungu wetu tubariki Mungu wetu atuongoze na tuseme aleluya daima na milele x2

  1. Mungu Baba tubariki Mungu mwana ‘tukomboe naye Roho Mtakatifu atuongoze daima

  2. Sadaka zetu mikononi matoleo kwako Baba, vyote vyako Mungu wetu tubariki daima

  3. Watoto wetu twatoa kwako kufanya kazi yako Mungu, watoto wako Mungu wetu wabariki daima

  4. Mali yote yatoka kwako mifugo, mimea pia kwako twasema sante Mungu wetu usifiwe daima

  5. Kaka dada usiachwe nyuma zawadi yako mikononi ili ujazwe Baraka tele kutoka kwake Mungu wetu.

  6. Ingawa wa Baba ni kidogo pokea zawadi zetu, tumetoa kulingana na uwezo wetu

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating

Recent Posts

bottom of page