top of page

Watakatifu wa Mbinguni

Updated: Dec 23, 2023


Watakatifu wa Mbinguni waimba nyimbo za shangwe Na malaika wake Mungu wanarukaruka kwa shangwe Natamani kwenda mbinguni, nikaimbe nyimbo za shangwe Nijiunge na malaika, nikaruke mbele za Mungu

  1. Ewe mpenzi wa moyo, ewe mlinzi wa roho, Roho yangu mimi, Nakusihi sana ewe somo wangu, nishike mkono Niongoze vyema nikajiunge nawe

  2. Ee malaika wa Mungu, shuka kutoka Mbinguni, Njoo kwangu mimi nakusihi sana nipe mbawa zako, na mimi niruke Nifike mbinguni nikajiunge nanyi

  3. Nyinyi mlioyashinda majaribu yake Mungu, Hapa duniani Twawasihi sana mkatuombee, na sisi tushinde Majaribu haya tukajiunge nanyi

  4. Matendo yaliyo mema, maneno yale mazuri, Moyo wa mapendo Zitaniongoza siku zangu zote, za maisha yangu Hadi nije huko nikajiunge nanyi

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating

Recent Posts

bottom of page