top of page

Waumini Simameni


  1. Waumini simameni - tupeleke neno lake Neno lake Bwana Mungu - ni nuru ya ulimwengu x2 Tulisome kweli (kweli kweli) Tulihubiri sana (biri sana) Tulisambaze kote na tulifundishe kweli Tulisome kweli (kweli kweli) Tulihubiri sana(biri sana) Tulisambaze kote na tulifundishe

  2. Ni neno la Bibilia - kutoka kwa Mungu Baba Anena kwa kinywa chake - na kwa maandiko yake x2

  3. Ni dawa ya mioyo yetu - tulizo kwa watu wote Tulipokeeni leo - tupate kunusurika x2

  4. Tuchezeni kwa furaha - nderemo na kwa vifijo Kwa ngoma na tarumbeta - kayamba hata vinanda x2

  5. Milima iyumbeyumbe - miti na ichezecheze Bahari ivume sana - mito ipige makofi x2

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating

Recent Posts

bottom of page