Yesu kwa Imani
- Hymns
- Nov 6, 2023
- 1 min read
Yesu kwa imani, nakutumaini, peke yako
Nishike sasa, na kunitakasa, ni wako kabisa
Tangu leo.
Nipe nguvu pia za kusaidia moyo wangu;
Ulikufa wewe, wokovu nipewe, nakupenda wewe,
Bwana wangu.
Hapa nazunguka katika mashaka, na matata;
Palipo na giza utaniongoza, hivi nitaweza,
Kufuata.

Comments