top of page

Yesu Mwana wa Mungu

Yesu Mwana wa Mungu x2, leo amefufuka. Piga vigelegele x2, leo amefufuka

  1. Yesu, Mwana wa Mungu, kweli amefufuka, ahadi yatimia, mzima amefufuka

  2. Kristu mshindaji mkubwa,ametupatanisha, na Babaye mbinguni, kwa damuye azizi

  3. Kristu Mwana-Kondoo, amechinjwa sadaka, tuile karamuye, tuimba aleluya

  4. Kristu mchungaji mwema, alitoa maisha, kwa ajili ya kondoo, mzima amefufuka

  5. Kristu aliuawa, katika udhaifu,anaishi daima, kwa nguvu yake Mungu

  6. Nendeni duniani, kuhubiri Injili, wote wabatizwao, mbingu wataurithi

  7. Nitawahubiria, ndugu zangu daima, jina lako tukufu, nitakusifu sana

  8. Leo ndio sikukuu, ilifanywa na Mungu, umefunguka mbingu, kwa ushindi wa Yesu

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating

Recent Posts

bottom of page