top of page

Zanena Siku Kuu

  • Hymns
  • Nov 11, 2023
  • 1 min read

Zanena, siku kuu, Kengele za juu, Waumini furahini, Mkombozi mkumbusheni Mzawa leo Bethlehemu Mzawa leo Bethlehemu


Ni hii leo, siku heri, Siku nzuri nzuri, Ya uasi kuondolewa, Ya mbingu kufunguliwa Yakisha maulaumu, Yakisha malaumu


Ni hii leo, siku njema, Siku ya salama, Aliposhuka Mwokozi, Mwanaye Mungu Mwenyezi Kuwa mwanadamu, Kuwa mwanadamu


Leo siku, hakika, Wala hamna shaka Kwamba dhambi ya asili, Yaweza kufutwa kweli Ina dawa timamu, Ina dawa timamu


Leo siku ya neema, Yameshuka mema Asifiwe Mungu juu, Watu wa imani kuu Waletewa amani, Waletewa amani

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating

Recent Posts

bottom of page